STEPHANIE OKEREKE ni muugizaji nyota wa NOLLYWOOD ambaye anakuja na movie yake ‘DRY’ambayo ameshirikiana na waigizaji wengine ambayo itakuwa inayoelezea kupinga ndoa za chini ya umri kwa watoto wa kike.
Stephanie aliandika kupitia blog yake kuhusu movie hiyo:"wanageria! ni wakati wa kutoa sauti zenu na kushirikisha mawazo,tunaitaji kumlinda mtoto wa kike kutoka katika unyanyasaji unaoendelea".
Turudi hapa kwetu bongo,wasanii wetu wa movie tumechoka na movie ambazo si halisi kwa maisha yetu, mnachoigiza hakina mapokeo chanya kwa jamii,kutwa mapenzi na starehe.
jamani bongo movie tuache! tuige kutoka kwa wasanii wa movies za nje wanavyofanya,ndio japo mapenzi yana run dunia duh sio kihivyo!!!
Tuwe na movies za kujenga sio kubomoa,kuna simulizi nyingi kuhusu maisha ya leo,ndio wadau wanataka,kufanikiwa kwa msanii wa movies sio kupata hela tu lahasha utaonaje raha pale movies zako zinapookoa jamii kuondokana kwa ukatili unaondelea kwa watoto?
Sasa bongomovies kazi kwenu kubadili simulizi ambazo zinaboa wakati mwingine tunaogopa hata kukaa na watoto,wazazi na watu tunaowaheshimu kisa simulizi zenu za mapenzi.
Habari bureeee hiyooo
No comments:
Post a Comment